Pata taarifa kuu
CAR-ICC-HAKI

Kiongozi wa zamani wa waasi wa Anti-balaka asafirishwa ICC

Mamlaka nchini Ufaransa imemkabidhi Patrice-Edouard Ngaïssona, kiongozi wa zamani wa wanamgambo wa Anti-balaka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Patrice Edouard Ngaissona, Waziri wa zamani wa Vijana na Michezo chini ya utawala wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize, ni mratibu wa kisiasa wa makundi ya kijeshi ya Anti-Balaka.
Patrice Edouard Ngaissona, Waziri wa zamani wa Vijana na Michezo chini ya utawala wa Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize, ni mratibu wa kisiasa wa makundi ya kijeshi ya Anti-Balaka. ISSOUF SANOGO/AFP/Getty
Matangazo ya kibiashara

Bw Ngaissona anashtumiwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ICC imesema katika taarifa yake.

Alikamatwa Desemba 12 kufuatia hati ya kukamatwa iliyotolewa na ICC "kwa kuhusika kwake kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanyika magharibi ya Jamhuri ya Afrika Kati ya Septemba 5, 2013 na mwezi Desemba 2014 ". Mahakama ya Ufaransa iliamuru Bw Ngaissona asafirishw mjini Hague.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikumbwa na machafuko mnamo mwezi Machi 2013 baada ya utawala kudhibitiwa na waasi wa Kiislam wa Seleka na kufanyiwa upinzani wa kijeshi na wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka.

Hata hivyo Patrice-Edouard Ngaissona, ambaye amekanusha tuhuma hizo dhidi yake, alichaguliwa mwezi Februari kwenye kamati tendaji ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), licha ya upinzani kutoka mashirika ya haki za binadamu kama vile Human Rights Watch.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.