Pata taarifa kuu
DRC-AU-EU-USHIRIKIANO

EU na AU kuendelea kushirikiana na DRC

Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika wametangaza Jumanne wiki hii kwamba wametambua hatua ya Mahakama ya Katiba ya kumtangaza Felix Tshisekedi kama rais wa DRC baada ya kutangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) mshindi wa uchaguzi wa Desemba 30 mwaka jana.

Rais Mteule wa DRC Felix Tshisekedi.
Rais Mteule wa DRC Felix Tshisekedi. REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya Uchaguzi wa urais yaliyopingwa na mgombea mwengine wa upinzani yalijadiliwa na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika katika mkutano wao mjini Brussels.

"Tumepokea hatua ya Mahakama ya Katiba," Federica Mogherini, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya anayehusika na Mambo ya Nje, Sera na Usalama amesem akatika mkutano na vyombo vya habari.

Ameongeza kuwa rais mpya wa DRC atakabiliana na "changamoto kubwa katika sekta mbalimbali" na kwamba atakuwa na jukumu la kuunganisha wananchi wa DRC. EU itaendelea kushirikiana kwa karibu na DRC, amesema Federica Mogherini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Richard Sezibera, pia amesema kuwa Umoja wa Afrika imetambua matokeo kamili ya Uchaguzi yaliyotangazwa na Mahakama ya Katiba. Umoja wa Afrika"bado una nia ya kuendelea na ushirikiano na na raia wa DRC ili kuendelea kukabiliana na changamoto zinazojitokeza," amesema Bw Sezibera.

Kamishna wa Umoja wa Afrika anayehusika na masuala ya Amani na Usalama, Smaïl Chergui, ambaye amezungumza baada ya Mogherini na Sezibera, amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na Tshisekedi na vyama vyote vya kisiasa nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.