Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Matokeo ya uchaguzi: Raia wa DRC wasubiri uamuzi wa Mahakama ya Katiba

Mahakama ya Katiba inaanza Jumanne hii Januari 15 kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais nchini DRC baada ya Felix Tshisekedi kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Desemba 30.

Martin Fayulu, akifikisha malalamiko yake katika Mahakama ya Katiba, Kinshasa Januari 12, 2019.
Martin Fayulu, akifikisha malalamiko yake katika Mahakama ya Katiba, Kinshasa Januari 12, 2019. REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Hayo ni baada ya mgombea mwengine wa upinzani kutoka muungano Lamuka Martin Fayulu kufungua kesi akipinga ushindi wa Tshisekedi.

Martin Fayulu anasema kumekuwa na njama ya kumuibia kura ili aonekane kuwa ameshindwa katika uchaguzi huo wa urais.

Anashtumu Tume ya Uchaguzi (CENI) pamoja na kambi ya Joseph Kabila kula njama na muungano wa upinzani CASH kumuangusha katika uchaguzi huo.

Wakati huo huo muungano wa upinzani CASH unasema unasubiri uamuzi wa Mahakama ya Katiba ili ufanye muungano na kambi ya rais joseph Kabila.

Mapema wiki hii Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Jumuiya ya nchi za kanda ya Maziwa Makuu ICGLR, zimetoa wito wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuendelea kwa mzozo kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais wa Desemba 30.

Hata hivyo wito huo umepokelewa kwa mikono miwili na baadhi ya wanasiasa nchini humo huku wengine wakiufutilia mbali,, wakishumu jumuiya hizo kuingilia katika masuala ya ndani ya DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.