Pata taarifa kuu
TUNISIA-MAANDAMANO-SAISA

Tunisia yaadhimisha siku utawala wa Ben Ali ulipoanguka

Leo Jumatatu Januari 14 ni siku ya mapumziko nchini Tunisia, kuadhimisha siku ambayo maandamano ya wananchi yalisababisha kuondoka madarakani kwa rais Zine el-Abidine Ben Ali, Januari 14 mwaka 2011.

Maandamano yaliibuka Tunisia kumshinikiza rais Zine el-Abidine Ben Ali kuondoka madarakani.
Maandamano yaliibuka Tunisia kumshinikiza rais Zine el-Abidine Ben Ali kuondoka madarakani. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo ya wiki nne, yalimalizika siku kama ya leo miaka minane iliyopita, baada ya kuchochewa na kijana Mohamed Bouazizi, aliyeamua kujiuawa kwa kujichoma kwa moto , kulalamikia ukosefu wa kazi nchini humo.

Miaka minane baadaye, baada ya maandamano hayo kusababisha vifo vya watu 340 na wengine zaidi ya 2000 kujeruhiwa, raia wengi bado wanaona walichokipigania bado hakijaonekana.

Mfuko wa bei umeendelea kuongezeka kwa asilimia nane, ukosefu wa kazi bado unashuhudiwa kwa asilimia 15 huku gharama ya maisha ikiendelea kupanda.

Hata hivyo, raia wa nchi hiyo wana jambo la kujivunia kuhusu demokrasia hasa uhuru wa kujieleza, suala ambalo halikuwepo miaka minane iliyopita.

Wananchi wa Tunisia wanapooadhimisha siku hii, wanataka ahadi zilizotolewa zitekelezwa ili maisha yao yabadilike.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.