Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Sudan yaendekea kukumbwa na Maandamano

Maandamano ya kumtaka rais wa Sudan Omar al-Bashir yanaendelea nchini humo. Vikosi vya kutuliza ghasia vimesambaratisha waandamanaji wanaopinga utawala wa rais Bashir ambao, siku ya Jumapili, walimiminika katika mitaa ya Khartoum na Darfur, ambapo mikusanyiko ilifanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa maandamano hayo dhidi ya serikali.

Maandamano katika mitaa ya Khartoum Januari 11, 2019.
Maandamano katika mitaa ya Khartoum Januari 11, 2019. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Waandaaji walitoa wito kwa maandamano mapya ya hasira.

"Mapinduzi ni chaguo la raia," waandamanaji wamekuwa wakiimba kwenye mitaa ya wilaya ya Bahari katika mji mkuu wa Sudan, kabla ya polisi kuingilia kati kuzima maandamano hayo, mashahidi waelimbaia shirika la Habari la AFP.

Wanawake wengi wameshiriki kataika maandamano hayo. Walitumia vifaa vya kujifunika nyuso zao kwa kujikinga na gesi ya machozi, mashahidi wamesema.

Waandamanaji walikuwa wamebebelea bendera ya Sudan na mabango ambayo yaliandikwa "amani, haki, uhuru", maneno ambayo yalitumiwa na waandamanaji yalipozuka maandamano hayo kwa mara ya kwanza tarehe 19 Desemba 2018, baada ya serikali kuamua kuongeza mara tatu bei ya mkate.

Katika nchi hiyo inayokumbwa na msukosuko wa kiuchumi, maandamano hayo haraka yaligeuka na kuwa maandamano yanayomtaka Rais Omar al-Bashir ajiuzulu.

Rais Bashir anatawala Sudan kwa mkono wa chuma tangu mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 1989.

Watu ishirini na wanne wameuawa tangu kuzuka kwa maandamano hayo, kulingana na ripoti rasmi. Hata hivyo shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International linasema watu zaidi ya 40 wameuawa katika maandamano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.