Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Omar Al Bashir: Sijafikia kuondoka madarakani

Rais wa Sudan Omar Al Bashir, anasema hataondoka madarakani licha ya shinikizo kutoka kwa waandamanaji wanaotaka aondoke, baada ya miaka 30 kuwa katika uongozi wa nchi hiyo.

Rais wa Sudan Omar Al Bashir alipokuwa akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 63 ya uhuru wa nchi yake, Desemba 31, 2018.
Rais wa Sudan Omar Al Bashir alipokuwa akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 63 ya uhuru wa nchi yake, Desemba 31, 2018. ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji nchini Sudan wanataka Bashir aondoke madarakani.

Waandamanaji wanaripotiwa kulenga na kuzichoma ofisi za chama cha Bashir na walitoa wito wa kumalizika utawala wake wa miaka 29.

Bashir aliingia madarakani katika mapinduzi ya jeshi mwaka 1989.

Siku ya Jumapili polisi wa kupambana na ghasia walifyatua gesi ya kutoa machozi kwa maelfu ya waandamanaji katika mji mkuu wa Sudan wakati wa maandamano yanayotoa wito kwa Rais Omar Al Bashir kujiuzulu yakiendelea kwa wiki ya tatu.

Hivi karibuni serikali ya Sudan ilisema watu 19 waliuwawa wakiwemo wafanyakazi wawili wa usalama tangu maandamano yalipoanza kaskazini-mashariki ya mji wa Atbara Desemba 19 mwaka 2018. Wakati huo huo kundi la kutetea haki za binadamu la Amnesty International lilieleza watu 37 wameuwawa katika ghasia hizo.

Maafisa wamefunga shule na kutangaza amri ya kutotoka nje na hali ya dharura nchini humo katika maeneo kadhaa tangu ghasia zilipoanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.