rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sudani Omar Al Bashir

Imechapishwa • Imehaririwa

Watatu wauawa katika maandamano Omdurman, Sudan

media
vikosi vya usalama vya Sudan vikijaribu kutawanya waandamanaji. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya polisi kuingilia kati kwa kutawanya maandamano ya kupinga serikali katika mji wa Omdurman, mji ulio karibu na mji mkuu wa Sudan, Khartoum, msemaji wa polisi amesema.


"Mkusanyiko uliopigwa marufuku ulifanyika Omdurman na polisi ilitawanywa waandamanaji kwa mabomu ya machozi," Hashim Abdelrahim msemaji wa polisi amesema katika taarifa hiyo.

"Kabla, polisi walitambua vifo vya waandamanaji watatu na umeanzisha uchunguzi," Bw Abdelrahim amesema bila kutoa maelezo zaidi.

Siku ya Jumatano, chanzo cha hospitali kiliambia shirika la Habari la AFP kwamba mtu mmoja alifariki kutokana na majeraha alioyapata wakati wa maandamano, huku watu sita wakijeruhiwa kwa risasi katika mji wa Omdurman.

Sudan inaendelea kukumbwa na maandamano kufuatia kupanda kwa bei ya mkate na mdororo wa uchumi unaoendelea. Kwa sasa waandamanaji wanaomba rais Omar Al Bashir ajiuzulu.