rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Madagascar Andry Rajoelina Marc Ravalomanana

Imechapishwa • Imehaririwa

Uchaguzi Madagascar: Rais mteule Rajoelina awataka wananchi kuijenga nchi yao

media
Andry Rajoelina mwenye makao makuu ya chama chake wakati wa hotuba yake ya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Katiba kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi Januari 8, 2019. RFI / Sarah T├ętaud

Baada ya Mahakama ya Katiba nchini Madagascar kumthibitisha mgombea Andry Rajoelina kama mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita, Rajoelina ametoa wito wa amani na kuwataka wananchi kuweka kando tofauti zao za kisiasa kuijenga nchi yao.


Andry Rajoelina alimshinda aliyekuwa mpinzani wake Marc Ravalomanana ambaye alifungua kesi katika mahakama hiyo.

Katika uchaguzi huo Rajoelina alipata ushindi wa asilimia 55.7 ya kura zote huku mpinzani wake Marc Ravalomanana akipata asilimia 44.3.

Juma lililopita Mahakama ya Katiba ilifutilia mbali rufaa ya Ravalomanana ikibaini kwamba madai yake hayana msingi.

Marc Ravalomanana anatarajiwa kuwahutubia wafuasi wake Jumatano wiki hii, lakini haijajulikana iwapo atakubali au la ushindi wa mpinzani wake.