Pata taarifa kuu
DRC-ZAMBIA-AFRIKA KUSINI-SIASA-USALAMA

Hali ya DRC kuzungumziwa katika mkutano wa marais wa Zambia na Afrika Kusini

Rais wa Zambia, Edgar Lungu yuko nchini Afrika Kusini kukutana kwa dharura na mwenyeji wake Cyril Ramaphosa ambapo watajadiliana kuhusu hali ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati huu wananchi wakisubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika Desemba 30 mwaka jana.

Mashine ya kupigia kura iliyotumiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Desemba 30, 2018 DRC.
Mashine ya kupigia kura iliyotumiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Desemba 30, 2018 DRC. John WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya ikulu ya Lusaka imethibitisha rais Lungu kwenda nchini Afrika Kusini kukutana na rais Ramaphosa.

Mkutano wao unafanyika wakati huu kinara wa upinzani kutoka vuguvugu la Lamuka, Martin Fayulu akiitaka tume ya uchaguzi CENI kutoa matokeo ya kweli ili kueousha vurugu zinazoweza kutokea ikiwa matokeo yatakuwa tofauti na matarajio ya wananchi.

Katika hatua nyingine chama kikuu cha upinzani nchini DRC, UDPS kimetoa ufafanuzi kuhusu kikao kilichofanyika jana kati ya mgombea wao Felix Tschisekedi na rais Joseph Kabila.

Katibu wa chama cha UDPS Jean-Marc Kabundi amesema wawili hao walizungumzia kuhusi haja ya kuboresha maridhiano.

Haya yanajiri wakati huu tume ya uchaguzi nchini humo ikitarajiwa kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi huo wakati wowote kuanzia sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.