Pata taarifa kuu
DRC-UNSC-SIASA-USALAMA

Uchaguzi DRC: Mkutano wa Baraza la Usalama la UN waahirishwa kwa ombi la Afrika Kusini

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeahirisha mkutano maalumu uliokuwa ufanyike juma hili kujadili uchaguzi mkuu uliofanyika nchini DRC, hatua ambayo ilitokana na ombi la nchi ya Afrika Kusini baada ya matokeo kuahirishwa kutangazwa.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatarajia kukutana juma hili kujadili hali inayoendelea DRC, baada ya ucahguzi wa Desemba 30.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatarajia kukutana juma hili kujadili hali inayoendelea DRC, baada ya ucahguzi wa Desemba 30. REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu maalumu wa baraza la usalama ulikuwa ufanyike hivi leo Jumanne lakini sasa umesogezwa mbele hadi siku ya Ijumaa, vyanzo kutoka kwenye Umoja wa Mataifa vimethibitisha.

Baraza hilo lilifanya mkutano kama huu ijumaa ya wiki iliyopita kufuatia maombi ya Ufaransa, lakini hata hivyo nchi wanachama zilishindwa kukubaliana kutoa taarifa ya pamoja kabla ya matokeo kutangazwa.

Nchi ya Afrika Kusini sambamba na Urusi pamoja na China zimetaka baraza hilo kutochukua hatua zozote hadi pale matokeo rasmi ya uchaguzi uliofanyika Desemba 30 yatakapotangazwa.

Tume ya uchaguzi nchini DRC, CENI, ilikuwa itangaze matokeo siku ya Jumapili ya wiki iliyopita lakini baadae ilitangaza kusogeza mbele bila kusema tarehe rasmi.

Jumuiya ya kimataifa ina imani kuwa matokeo ya uchaguzi huu yatamaliza miaka zaidi ya 40 kwa taifa hilo kushuhudia viongozi wakibadilishana madarakani kwa amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.