Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Kanisa Katoliki DRC: Tunafahamu mshindi wa uchaguzi

Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Cenco) limesema kuwa linafahamu jina la mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Desemba 30 nchini DRC na kuomba Tume ya Uchaguzi (CENI) kutangaza matokeo katika hali ya "ukweli na haki ".

Baraza Kuu la MAaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC laionya Tume ya Uchaguzi CENI.
Baraza Kuu la MAaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC laionya Tume ya Uchaguzi CENI. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Baraza hilo limesema lina sampoli ya wawakilishi iliyochapishwa katika vituo vya kupigia kura ambavyo vinawauhusu kujuwa jina la rais aliechaguliwa. Sampuli hiyo ni ya vituo zaidi ya elfu 23 kati ya vituo elfu 70 vilivyowekwa na Ceni.

Donatien Nshole, msemaji wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC amesema sio jukumu lao kutangaza matokeo wao ni waangalizi lakini wanafahamu nani aliechaguliwa na wananchi.

Padri Donatien Nshole, Msemaji wa baraza Kuu la maaskofu wa Kanisa Katoliki DRC (CENCO) akisoma ujumbe wa Maaskofu wa DRC.
Padri Donatien Nshole, Msemaji wa baraza Kuu la maaskofu wa Kanisa Katoliki DRC (CENCO) akisoma ujumbe wa Maaskofu wa DRC. RFI/Sonia Rolley

"Ni muhimu kusisitiza kuwa kasoro zilizojitokeza haziwezi kuathiri kwa kiwango kikubwa chaguo la wananchi wa DRC walioonyesha wazi katika uchaguzi wa urais wa Desemba 30," msemaji wa Cenco ameongeza."

Cenco imeitaka Tume ya Uchaguzi (CENI) kama taasisi inayounga mkono demokrasia kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa heshima ya ukweli na haki," amesema Padri Nshole.

Msemaji wa Baraza Kuu la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC (Cenco) amekuwa anawasilisha ripoti ya awali ya ujumbe wa waangalizi wa Uchaguzi wa Tume ya Haki na Amani ya Cenco, ambayo inasema kuwa ilikuwa na waangalizi 40,000 wakati wa uchaguzi wa siku ya Jumapili.

Uchaguzi Mkuu wa Jumapili utapelekea kumpata mrithi wa Rais Joseph Kabila, ambaye hakuruhusiwa kuwania muhula wa tatu kulingana na Katiba.

Siku ya Jumanne CENI ilisema kuwa itatangaza matokeo ya awali siku ya Jumapili Januari 6, 2019. Siku ay Alhamisi CENI ilisema kuwa kuna uwezekano zoezi hilo liahirishwe.

Raia nchini DRC bado wanasubiri kutangazwa matokeoa ya uchaguzi huo.

hali ya wasiwasi bado inaendelea, huku huduma ya intaneti ikiendelea kufungwa na mitambo ya radio ya kimataifa RFI ikizimwa.

Wakati huo huo Tume ya Uchaguzi CENI imesema kuwa tayari imehesabu asilimia 20 tu ya kura zilizopigwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.