Pata taarifa kuu
DRCUNSC-SIASA-USALAMA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kujadili uchaguzi wa DRC

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo Ijumaa jijini NewYork Marekani kujadili juu ya mustakabali wa taifa la Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakati huu wananchi katika nchi hiyo wakisubiri kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili Desemba 30, 2018.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatarajia kukutana kujadili hali inayoendelea DRC.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanatarajia kukutana kujadili hali inayoendelea DRC. REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Baraza hili linakutana wakati Mweneykiti wa Tume ya uchaguzi ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI), Cornelle Nangaa amenukuliwa na vyombo vya habari jijini Kinshasa akisema kuwa huenda kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi kukuahirisha wakati huu wafanyakazi wa tume hiyo wakiendelea kukukusanya kura kutoka maeneo kadhaa nchini humo.

Katika taarifa yake hii leo mwenyekiti wa CENI Corneille Nangaa amesema kwa sasa tume haitaweza kutangaza matokeo ya awali Januari 6 kama ilivyokuwa imepangwa huku akisema kuwa kazi ya kukusanya masanduku ni kubwa na bado haijakamilika, kutokana na ukubwa wa nchi pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo mpaka sasa.

Hata hivyo wanasiasa huko DRC wameendelea kuishutumu serikali ya Congo kwa kushindwa kufungua huduma ya intaneti na kuzuia vyombo vya habari vya kimataifa ikiwemo RFI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.