rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Somalia AMISOM UN Al Shabab

Imechapishwa • Imehaririwa

Kambi kuu ya Umoja wa Mataifa yashambuliwa Somalia

media
Askari wa AMISOM wakipiga doria mbele ya Msikiti Mogadishu, mji mkuu wa Somalia. REUTERS/Ismail Taxta

Kambi kuu ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, imeshambuliwa kwa mabomu. Watu watatu wamejeruhiwa kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.


"Mambomu saba yamedondoka ndani ya kambi moja kuu ya Umoja wa Mataifa, na kujeruhi wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa na mpita njia," Umoja wa Mataifa umesema katika taarifa yake. "Wfanyakazi waliojeruhiwa wanaendelea vizuri," Umoja wa Mataifa umeomgeza.

Kundi la wapiganaji wa Al-Shabab, lenye mafungamano na Al Qaeda, limekiri kuhusika na shambulio hilo.

Al-Shebab inaendelea vita nchini Somalia kwa lengo la kuiangusha serikali ya nchi hiyo wenye askari dhaifu inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

Awali mashambulizi kama hayo yalikuwa yakitokea karibu kila kukicha, lakini kwa sasa yamepungua tangu wapiganaji wa kundi hilo kuondoka kwenye ngome zao huko Mogadishu mnamo mwaka 2011.

Al-Shabab bado inadhibiti maeneo ya vijijini, bila hofu yoyote, na hufanya mashambulizi dhidi ya majengo ya serikali, maafisa wa serikali, jeshi na raia huko Mogadishu na pia katika miji mingine ya Somalia.