Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-UCHAGUZI-KURA

DRC: Gavana wa jimbo la Mbuji Mayi atuhumiwa kuvuruga zoezi la kuhesabu kura

Wakati zoezi la kuhesabu kura likindelea katika maeneo mbalimbali nchini DRC huku  zoezi hili likikamilika katika miji kadhaa ya Mbandaka, Bunia na Ituri, wakati huu wafuasi wa chama kikuu cha upinzani UDPS wamemtuhumu Gavana wa jimbo la Mbuji Mayi, Ngoy Kasanja kuwatumia vijana kwa kuwapa pesa ili kuvuruga zoezi la kuhesabu kura.

Zoezi la kupiga kura lilivyofanyika Desemba 30 2018
Zoezi la kupiga kura lilivyofanyika Desemba 30 2018 © Caroline Thirion / AFP
Matangazo ya kibiashara

Chama hicho cha UDPS katika mkoa huo kimethibitisha kuwa vijana hao walioajiriwa na Gavana na kufahamika kama San pur san, walivamia kituo cha kuhesabu kura na kuchana karatasi za matokeo ya uchaguzi.

“Tunasikitishwa na kitendo cha kufukuzwa kwa waangalizi na baadhi ya mashahidi katika baadhi ya vituo vya kupigia kura hapa Lubumbashi, "  amesema Florent Ngandu mwenyekiti wa tawi la vijana wa chama cha UDPS

"Waangalizi wetu walipita hapa asubuhi, lakini hawakuruhisiwa kuingia katika ofisi hizo, kwa sababu kulikuwa Polisi ambao hawakuwaruhusu kuingia kushuhudia kilichokuwa kinaendelea," aliongeza.

Tuhuma hzo zimetupiliwa mbali na Gavana wa Jimbo la Mbuji May Ngoy Kasonji ambae amesema vijana wa chama cha UDPS ndio wanaosababisha vurugu.

“Kile ninachoweza kusema ni kwamba tumezoea uongo mwingi kutoka kwa watu wa UDPS. Hapa tuna wafuasi wa FCC na UDPS, sisi ndio waathiriwa, hawawezi kututuhumu," ameongeza.

Hayo yanajiri wakati Kanisa Katoliki kupitia Tume yake ya sheria na amani ambayo ilikuwa na waangalizi 738 katika jimbo la Lubumbashi, linalaumu kuona baadhi ya waangalizi wake walizuiliwa kuingia katika vituo vya kupigia kura na hata wakati wa zoezi la kuhesabu kura.

“Tunatuhumu vitendo vya vurugu viliyotekelezwa na vijana walioajiriwa na Gavana Ngoy Kasanji ambaye anawaita wanaye. Wanafahamika kwa jina la 100% hawataki watu waandike matokeo ya uchaguzi katika vituo mbalimbali" amesema Padri Benoit Mukwanga Mwana Tambwe Katibu Mkuu wa Tume ya sheria na amani mjini Lubumbashi.

Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge wa mkoa na kitaifa, yamepangwa kutangazwa Januari 6 mwaka huu wakati huu serikali ya DRC ikiendelea kuzuia matumizi ya Internet licha ya wito kutoka nchi za Magharibi kuitaka kuwaacha wananchi kutumia mitandao ya kijamii.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.