Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DRC-JOSEPH KABILA-CENI

Unayopaswa kuyajua kuhusu DRC

Mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaendelea kupiga kura katika maeneo mbalimbali nchini humo, kumchagua rais atakayerithi kiti cha Joseph Kabila.

Wagombea wakuu wa urais nchini DRC, Martin Fayulu (Kushoto), Emmanuel Ramazani Shadary (Katikati) na Felix Tshisekedi (Kulia)
Wagombea wakuu wa urais nchini DRC, Martin Fayulu (Kushoto), Emmanuel Ramazani Shadary (Katikati) na Felix Tshisekedi (Kulia) AFP
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo, uliocheleweshwa kwa miaka miwili utamaliza utawala wa miaka 18 wa Rais Joseph Kabila, aliyeingia madarakani mwaka 2001 baada ya kuuawa kwa baba yake Laurent Kabila.

Dondoo muhimu kuhusu uchaguzi huo

Raia milioni 46 walijiandikisha kushiriki uchaguzi huo kumrithi Joseph Kabila aliyepo uongozini kwa miaka 18.

Alichukua madaraka Januari 2001 akiwa na umri wa miaka 29.

DRC haijawahi kushuhudia ubadilishanaji wa madaraka tangu ilipopata uhuru mwaka 1960 kutoka kwa Mkoloni, mbelgiji.

Mobuto Seseseko Kukungwendu wa Zagamba, alitawala nchi kwa miaka 30 (wakati huo ikiitwa Zaire) kabla ya kufurushwa na Laurent Kabila akisaidiwa na majeshi ya Uganda na Rwanda, 1997

Wagombea 17 wanawania kiti cha urais akiwemo mwanamama, Marie-Josée Ifoku

Awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyike Disemba 23 lakini Tume ya uchaguzi Ceni iliahirisha kwa sababu ya usalama mdogo.

Miji ya beni na Goma, iliyopo mashariki na Mji wa Yumbi uliopo magharibi haishiriki uchaguzi kwa kile serikali inasema usalama mdogo mapigano ya kikoo na ugonjwa wa ebola. Tume inasema uchaguzi katika maeneo hayo utafanyika machi 2019.

Aidha kuhusu usalama mdogo Shirika la Misaada la Norway linasema hjado kufikia 2018 ukosefu wa usalama umepelekea zaidi ya watu milioni 1.7 kuyakimbia makazi yao.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo watu 5500 hukimbia makwao kila uchao.

Umoja wa Mataifa una idadi kubwa ya wanajeshi wakulinda amani nchini DRC, kupitia kikosi chake cha Monusco, inakadiriwa kuwa 18,000.

Uchaguzi katika eneo la Yumbi, Jimboni Bandundu Magharibi umeahirishwa kwa kile Tume ya Uchaguzi Ceni inasema mapigano ya koo ambayo yamegharimu maisha ya watu 100.

Uchaguzi huu pia unatajwa kuwa jaribio la demokrasia kwa taifa hilo lenye raslimali lukuki.

Wagombea watatu wanaochuana vikali kuwania kiti cha urais ni Ramadhan Shadary wa chama tawala FCC, Martin Fayulu wa Lamuka na Felix Tchisekedi wa UDPS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.