Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Askari 13 wauawa katika shambulizi la kushtukiza Nigeria

Magaidi wa Boko Haram wamewauwa wanajeshi 13 na polisi mmoja Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Vikosi vya ulinzi na usalama vimekuwa vikiliengwa na mashambulizi ya makundi mbalimbali ya watu wenye silaha nchini humo.

Askari wa jeshi la Nigeria wakipambana na makundi ya magaidi.
Askari wa jeshi la Nigeria wakipambana na makundi ya magaidi. STEFAN HEUNIS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, wapiganaji wa Boko Haram walivamia msafara wa wanajeshi katika barabara kuu ya Maiduguri kwenda Borno.

Mbali na hilo, magaidi hao walijaribu pia kuvamia kambi ya jeshi katika eneo hilo. Boko Haram katika siku za hivi karivuni imeongeza mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya wanjashi wa Nigeria.

Katikatiya mwezi Novemba Askari wapatao 100 wa jeshi la Nigeria akiwemo afisa wa ngazi za juu wa jeshi hilo waliuawa katika shambulio dhidi ya kituo cha jeshi, ambapo duru za usalama zilisema, lilifanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu Afrika Magharibi.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na duru za usalama, shambulio hilo liliendeshwa dhidi ya kambi ya jeshi iliyopo kwenye kijiji cha Metele katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambacho ni kitovu cha uasi ulioanzishwa na kundi la kigaidi la Boko Haram na jengine la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu lililojitenga na kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.