Pata taarifa kuu
DRC-SADC-ICGLR-SIASA-USALAMA

Mkutano wa kikanda kuhusu DRC kufanyika Brazzaville

Mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Maendeleo ya Kiuchumi Kusini mwa bara la Afrika SADEC na nchi za Maziwa Makuu ICGLR unafanyika leo jijini Brazzaville nchini Congo.

Rais wa Congo Denis Sassou-Nguesso, Januari 22, 2015.
Rais wa Congo Denis Sassou-Nguesso, Januari 22, 2015. REUTERS/Anis Mili
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa nchi hizo watajadili kuhusu hali ya kisiasa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kuelekea uchaguzi wa Desemba 30 mwaka huu.

Tangazo la mkutano huo lilitolewa tarehe 21 Desemba na Namibia, ambayo inaongoza kwa sasa SADC baada ya ziara ya maandalizi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo, Jean-Claude Gakosso.

Ikiwa zimesalia siku tatu kabla ya uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na baada ya kampeni iliyogubikwa na vurugu, Brazzaville inasema ina wasiwasi juu ya hatari ya kuibuka mgogoro wa baada ya uchaguzi, na hali hiyo inaweza kuhatarisha hali ya usalama katika kanda nzima.

Serikali ya Brazzaville inasema inataka kutoa ujumbe wa kuvumiliana na kujiepusha na machafuko kwa wadau wote katika mchakato wa uchaguzi nchini DRC.

Marais watano tayari wamethibitisha kuwa watahudhuria mkutano huo. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, anayehusika kwa mstari wa mbele katika mchakato wa uchaguzi nchini DRC, Rais wa Namibia Hage Geingob, ambaye ni rais wa sasa wa SADC, Rais wa Zambia Edgar Lungu , mwenekiti wa kitengo cha ulinzi na usalama katika jumuiya hiyo, Rais wa Botswana Masisi, na Rais wa Angola João Lourenço watahudhiria mkutano huo. Rwanda na Uganda zitawakilishwa na mawaziri wao wa mambo ya kigeni.

Wapinzani wa DRC wamesema wanatarajia mengi kutoka mkutano huu ili kusaidia kupata mwafaka katika mzozo wa kisiasa nchini mwao na kuishinikiza Tume ya Uchaguzi kuhakikisha kuwa Uchaguzi huo unakuwa huru na haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.