Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-CENI-MASHINE

CENI imejiandaa kwa Uchaguzi Mkuu siku ya Jumapili nchini DRC ?

Bado kuna maswali mengi kuhusu utayari wa nchini ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanikisha Uchaguzi Mkuu siku ya Jumapili, baada ya zoezi hilo kuahirishwa kwa wiki moja. 

Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) imeonyesha mashine ya kupigia kura itakayotumika katika uchaguzi wa Desemba 23.
Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi (CENI) imeonyesha mashine ya kupigia kura itakayotumika katika uchaguzi wa Desemba 23. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, Tume ya Uchaguzi CENI, ilitangaza kuahirisha uchaguzi huo kwa wiki moja kutoka tarehe 23 hadi tarehe 30 Desemba, baada ya kuteketea kwa jengo ambalo lilikuwa limehifadhi vifaa vya kupigia kura katika jiji kuu, Kinshasa.

Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa ulisema uko tayari kuisaidia Tume ya Uchaguzi, kuhakikisha kuwa kuna usalama, na vifaa vya kupigia kura vinakuwa salama, usaidizi ambao serikali ya Kinshasa umekataa.

Ijumaa iliyopita, Joseph Olenghankoy, rais wa Tume ya serikali inayothathmini maandalizi ya Uchaguzi huo, ameitaka serikali kuruhusu usaidizi kutoka kwa MONUSCO.

Hata hivyo, msemaji wa CENI ambaye hakutaka kufahamika, amesema tume ya Uchaguzi itaomba msaada kutoka kwa MONUSCO iwapo itaona ni vema kufanya hivyo, lakini kwa sasa haina nia ya kufanya hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.