Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Kumi na saba wauawa katika shambulio kaskazini mwa Nigeria

Watu kumi saba wameuawa katika kijiji cha Zamfara, Kaskazinii mwa Nigeria mwishoni mwa wiki hii iliyopita, kwa mujibu wa polisi na mashahidi. Shambulio hilo lilitokea siku chache baada ya mashambulizi mengine yanayofanana katika vijiji viwili, mashambulizi ambayo yaligharimu maisha ya watu 25.

Ni Magami, katika Jimbo la Zamfara kaskazini mwa Nigeria ambapo kulitokea shambulio ambalo liliwaua watu 17 Jumamosi, Desemba 22, 2018.
Ni Magami, katika Jimbo la Zamfara kaskazini mwa Nigeria ambapo kulitokea shambulio ambalo liliwaua watu 17 Jumamosi, Desemba 22, 2018. Carte/ RFI
Matangazo ya kibiashara

Watu wenye silaha waliowasili kwenye pikipiki siku ya Jumamosi wakitokea katika kijiji cha Magami, wawalifyatulia risasi wakazi waliokuwa wakitoroka makaazi yao. "Baada ya shambulio, tuliokota miili 17 ambayo ilizikwa," Kasimu Bello, mkazi wa Magami, ameliambia shirika la Habari la AFP.

Mkazi mwingine wa Magami, Umaru Bawa, amethibitisha shambulio hilo, akiongeza kuwa "Majambazi waliwafukuzia watu waliokuwa wakitoroka makazi yao na kuwaua kwa kuwapiga risasi."

Msemaji wa Polisi katika Jimbo la Zamfara Mohammed Shehu amesema vijana wake watawakamatwa na "kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wahusika wa kitendo hicho cha kikatili".

Desemba 21, watu wasiopungua 25 waliuawa katika mashambulizi dhidi ya vijiji viwili na makundi ya watu wenye silaha ambao walikuwa wezi wa mifugo, wanaoendelea kuhatarisha usalama kaskazini mwa Nigeria, kwa mujibu wa vyanzo vya polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.