Pata taarifa kuu
DRC-ADF NALU-USALAMA-ICHAGUZI-EBOLA

DRC: Watu nane akiwemo mwanajeshi wauawa Beni baada ya kushambuliwa na ADF NALU

Waasi wanaoaminiwa kuwa wa ADF NALU wamewauwa watu wanane, wakiwemo watoto watu, Wilayani Beni Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na kuzua hofu kuelekea Uchaguzi wa Jumapili.

Wanajeshi wa DRC, wakiwa Mashariki wma DRC.
Wanajeshi wa DRC, wakiwa Mashariki wma DRC. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Awali shirika la Habari la Ufaransa AFP, liliripoti kuwa watu watano akiwemo mwanajeshi waliuawa baada ya kushambuliwa na ADF NALU. Mauaji hayo yalitokea Jumapili alfajiri katika eneo la Masiani.

Ripoti zinasema kuwa, watu wengine watatu wamejeruhiwa na wanaendelea kupokea matibabu.

Mauaji haya yamekuja wakati huu nchi hiyo ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu Jumapili ijayo lakini pia wilaya ya Beni likiendelea kukabiliwa na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Kuna wasiwasi kuwa makundi ya waasi kama ADF huenda yakatatiza Uchaguzi katika Wilaya hiyo kwa kuwavamia wapiga kura na maafisa wa Tume ya Uchaguzi lakini pia Shirika la agya duniani WHO linasema maambukizi ya Ebola yanaendelea kushuhudiwa kutokana na utovu wa usalama.

ADF NALU ni waasi waliokimbia nchini DRC mwaka 1995, baada ya kufukuzwa nchini Uganda, baada ya jaribio la kumwondoa raia Yoweri Museveni kugonga mwamba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.