Pata taarifa kuu
MALI-NIGER-BARKHANE-USALAMA

Wanamgambo sita wa Kiislamu wauawa katika mashambulizi ya anga Mali

Wapiganaji zaidi sita wa Kiislamu walio kuwa kwenye pikipiki karibu na mpaka wa Mali na Niger, wameuawa na kikosi cha askari wa Ufaransa Barkhane usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii, kwa mujibu wa msemaji wa makao makuu ya jeshi la Ufaransa.

Askari wa Ufaransa katikati mwa Mali, Novemba 1, 2017.
Askari wa Ufaransa katikati mwa Mali, Novemba 1, 2017. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari, Kanali Patrick Steiger amesema wapiganaji wasiopungua sita wa kundi la kigaidi wameangamizwa na pikipiki tano kuharibiwa bibaya.

"Operesheni ilianza wakati kundi la wapiganaji waliokuwa kwenye pikipiki nane walionekana huko Niger. Walifuatiliwa mara moja na ndege isio kuwa na rubani inayohusika na ukaguzi.

"Kwa hiyo ilionekana kuwa wapiganaji hao walivuka mpaka na kuingia nchini Mali," alisema msemaji wa makao makuu ya jshi la Ufaransa, "pamoja na kuamua hali ya kigaidi ya kundi hili," na hivyo kujua vigezo ambavyo hakuvitaja vilivyoashiria kundi hilo kuwa ni la kigaidi.

Wapiganaji wa Kiislamu wameacha kutumia magari katika operesheni zao na hivyo kutumia pikipiki kwa kujirahisishia katika harakati zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.