rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

CAR

Imechapishwa • Imehaririwa

Zoezi la kuwapokonya silaha wapiganaji laanza Jamhuri ya Afrika ya Kati

media
Wapiganaji wa kundi la zamani la Seleka katika mitaa ya Bangui, Januari 27, 2014. REUTERS/Siegfried Modola

Hatimae nchi ya Jamuhuri ya Afrika ya kati imeanza mpango wa kuwapokonya silaha wapiganaji na kuwarejesha katika maisha ya kawaida, baada ya kuahirishwa kwa mara kadhaa huko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ambako bado sehemu kubwa inashikiliwa na makundi yanayomiliki silaha.


Mpango huo utawahusisha wapiganaji takriban mia tano kutoka makundi ya RJ, Revolution Justice tawi na Sayo na Tawi la Belanga, makundi mawili hasimu ya Anti Balaka katika eneo hilo la kaskazini magharibiu mwa Jamuhuri ya Afrika ya kati.

Idadi ambayo inaelezwa kuwa ndogo ukilinganisha na idadi ya makundi ya wapiganaji wanakadiriwa kufikia elfu 45.

Hata hivyo Jean Willybiro Sako, waziri wa zamani na mgombea kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka 2015 amesema anamatumaini kwamba mpango huo utafaulu.

Mradi huo wenye thamani ya dola milioni 30 umedhaminiwa na benki ya dunia na unatarajia kuwarejesha katika maisha ya kawaida jumla ya wapiganaji elfu saba.