Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-ERITREA-USHIRIKIANO

Ethiopia yaondoa jeshi lake kwenye mpaka wenye mzozo na Eritrea

Nchi ya Ethiopia imethibitisha kuwa imeanza kuwaondoa wanajeshi wake kwenye mpaka wenye utata na jirani yake nchi ya Eritrea kama sehemu ya utekelezaji wa makubaliano yaliyotiwa saini baina ya nchi hizo mwezi Julai mwaka huu.

Ethiopia imeanza kuwaondoa wanajeshi wake kwenye mpaka unaozozaniwa na Eritrea.
Ethiopia imeanza kuwaondoa wanajeshi wake kwenye mpaka unaozozaniwa na Eritrea. (Photo : Manu Pochez/ RFI)
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano haya yalimaliza miongo miwili ya mzozo wa kimipaka ulioshuhudia maelfu ya raia wakipoteza maisha.

Kuondolewa kwa wanajeshi wa Ethiopia kwenye mpaka huo limekuwa ndio takwa kubwa la utawala wa Asmara.

Nchi hizi mbili zilipigana vita kati ya mwaka 1998 na 2000 ambapo licha ya kufikiwa kwa makubaliano ya amani miaka miwili baadae, uhusiano baina ya nchi hizi mbili ulikuwa wa utata mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.