rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Cameroon Paul Biya

Imechapishwa • Imehaririwa

Paul Biya atoa msamaha kwa wanaharakati 289 waliokuwa wanakabiliwa na mkono wa sheria

media
Mji wa Buea,katika maoja ya majimbo yanayozungumza Kiingereza, Cameroon, Aprili 27, 2018. ALEXIS HUGUET / AFP

Rais wa Cameroon, Paul Biya ameagiza kusitishwa kunyongwa kwa zaidi ya watu 289, wengi wao wakiwa ni wanaharakati wa vuguvugu linalotaka kujitenga kutoka eneo la kaskazini na kusini mwa nchi hiyo ambako wananchi wake wanazungumza Kingereza.


Tangu kuanza kwa harakati za eneo hilo kujitenga vyombo vya usalama nchini Cameroon vimekuwa vikiendesha msako dhidi ya watu inaodai wamekuwa wakishirikiana na makundi ya kijihadi kutatiza usalama kwenye eneo hilo kwa kuwaua wanajeshi.

Rais Biya pia ametangaza msamaha kwa mamia ya wafungwa wa kisiasa. Ngnie Kamga ni mwenyekiti wa jukwaa la wanasheria nchini Cameroon.

Tangazo la rais Biya limekuja ikiwa ni miezi michache tu imepita tangu achaguliwe kwa mara nyingine katika uchaguzi ambao ulikashifiwa na upinzani.