Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI-USALAMA

Uchaguzi DRC: Makabiliano yatokea kati ya wafuasi Kindu

Kampeni ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kukabiliwa na sintofahamu na mvutano kati ya wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini humo.

Mgombea wa upinzani Martin Fayulu Goma, Desemba 6, 2018.
Mgombea wa upinzani Martin Fayulu Goma, Desemba 6, 2018. © REUTERS/Samuel Mambo
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili kulitokea machafuko katika mji wa Kindu, ngome ya chama tawala na washirika wake ambako mgombea wa upinzani anadai kuwa aliamua kusitisha kuendesha kampeni yake, vyanzo kadhaa vimeripoti.

Machafuko yaliyotokea katika eneo la Kindu katika mkoa wa Maniema yamesababisha "watu wanne kujeruhiwa vibaya, ikia ni pamoja na watu wanne waliojeruhiwa kwa risasi," shirika moja la haki za binadamu la Acaj limebaini kwenye ukurasa wake wa Twitter, huku likisema kuwa lilikuwa na waangalizi wake katika eneo la tukio.

Wafuasi wa mgombea wa upinzani Martin Fayulu, aliokuwa anatarajiwa siku ya Jumapili katika mji wa Kindu kwa mkutano wa uchaguzi, walikabiliana na watu wanaodai kuwa wafuasi wa muungano wa vyama vinavyoshiriki serikalini (FCC), ambavyo vinamuunga mkono rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila na mgombea wake Emmanuel Ramazani Shadary, kutoka Maniema.

Wafuasi wa Martin Fayulu "walishambuliwa na makundi ya vijana wanaodai" kuwa wafuasi wa FCC na kusema kuwa "walitaka kumzuia Fayulu asiendeshi mkutano wake katika mji huo," kiongozi wa Acaj, Wakili Georges Kapiamba ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Waangalizi wetu waliona jinsi vikosi vya usalama vikipuuzia mwenendo hatari wa wafuasi wa chama tawala na washirika wake. Badala ya kuwazuia waliwasambaratisha wafuasi wa Fayulu kwenye uwanja wa ndege," Kapimba ameliambia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.