Pata taarifa kuu
DRC-UGANDA-UCHUMI

Daraja linalounganisha Kivu Kaskazini na Uganda lavunjika, uchumi matatani Beni

Wafanyabiasaha katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC wameelezea masikitiko yao kufuatia kuvunjika kwa daraja linalounganisha mkoa wa Kivu Kaskazini na Uganda. Tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili.

Mtoto akicheza karibu na daraja lililovunjika kufuatia mafuriko mjini Kampala Mei 8, 2013. (Picha ya inayoashiria tukio lililotokea)
Mtoto akicheza karibu na daraja lililovunjika kufuatia mafuriko mjini Kampala Mei 8, 2013. (Picha ya inayoashiria tukio lililotokea) © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Daraja la Lubihira katika mji wa Beni unaoendelea kuathirika na ugonjwa wa Ebola na mashambulizi ya hapa na pale ya kundi la waasi wa Uganda wa ADF lilivunjika.

Mashahidi wanasema daraja hilo lilivunjika wakati lori kubwa aina ya Actros lilikuwa likipita likitokea nchini Uganda. Taarifa hii imethibitishwa na afisa wa serikali katika eneo hilo, Donat Kibwana, akiliambia shirika la Habari la AFP.

"Kwa sasa, tunajaribu kuangalia jinsi ya kuokoa hali kwa kusubiri ukarabati. Vinginevyo mkoa wote kuna hatari ukabiliwe na baa la njaa kwa sababu daraja hili lilikuwa linaounganisha eneo la Mashariki mwa DRC na Uganda na Tanzania," Bw Kibwana ameongeza.

"Eneo hili la mpakani ni muhimu sana kwetu na kwa DRC kwa ujumla. Bidhaa nyingi mahitajio kwa raia wa mkoa wa Kivu Kaskazini hutoka Uganda na huingia nchini hapa kupitia daraja hili," amesema Naibu kiongozi wa shirika la wafanyabiashara la FEC, Cléophace Paluku.

Mwezi Januari 2017, kuvunjika kwa daraja la Semuliki linalounganisha DRC na Uganda kulisababisha bei za bidhaa mahitajio kupanda mara dufu katika mji wa Beni, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.