Pata taarifa kuu
SOMALIA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Marekani yarejesha ubalozi wake Somalia

Marekani imerejesha Ubalozi wake nchini Somalia, kwa mara ya kwanza baada karibu miaka 30. Wizara ya Mambo ya nje imesema, hatua hii imefikiwa, kutokana na juhudi za kiusalama na kisiasa zilizopigwa katika taifa hilo.

Marekani yarejesha ubalozi wake Somalia lakini hali ya usalama bado haijadhibitiwa na mashambulio ya mara kwa mara ya kundi la al-Shabab huripotiwa, hasa Mogadishu.
Marekani yarejesha ubalozi wake Somalia lakini hali ya usalama bado haijadhibitiwa na mashambulio ya mara kwa mara ya kundi la al-Shabab huripotiwa, hasa Mogadishu. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kuhusu kufunguliwa kwa ubalozi huo, Waziri Msaidizi wa mambo ya nje wa Marekani, Wendy Sherman anayehusika na maswala ya kisiasa., " Ishara ya kuimarika kwa uhusiano baina ya Marekani na Somalia." Sherman aliendelea kusema kuwa kufunguliwa kwa ubalozi huo pia ni ishara ya kuwa Marekani ina imani yakwamba Somalia, ambayo imeharibiwa na vita, itaweza kupata utulivu na kufikia malengo yake.

Balozi wa Marekani, ambaye makazi yake yamekuwa jijini Nairobi nchini Kenya, anatarajiwa kuhamia mjini Mogadishu.

Marekani ilifunga Ubalozi wake nchini Soamlia mwaka 1991, baada ya kuzuka kwa vita kati ya waasi na wanajeshi wa serikali.

Uhusiano kati ya Somalia na Marekani umekuwa ukiimarika tangu Agosti 2012, Somalia ilipofikisha kikomo kipindi cha mpito na kuteua viongozi wapya.

Rais Obama aliteua balozi wa kwanza wa Marekani Somalia Februari mwaka huu, na miezi miwili baadaye waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry akawa waziri wa kwanza wa kigeni wa Marekani kuzuru Mogadishu.

Somalia nayo iliteua balozi wa kuiwakilisha Marekani.

Licha ya hatua hiyo inayoashiria kuimarika kwa hali Somalia, hali ya usalama bado haijadhibitiwa na mashambulio ya mara kwa mara ya kundi la al-Shabab huripotiwa, hasa Mogadishu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.