rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Algeria Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz al-Saud

Imechapishwa • Imehaririwa

Mwanamfalme wa Saudia aendelea na ziara yake Afrika

media
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz (kushoto) akimpokea Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman aliwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Nouakchott Desemba 2, 2018. © Bandar AL-JALOUD / Saudi Royal Palace / AFP

Mwanamfalme wa Saudia Arabia Mohamed Bin Salman ameelekea nchini Algeria baada ya ziara ya saa kadhaa nchini Mauritania ambapo alikutana na rais wa nchi hiyo Mohamed Ould Abdel Aziz.


Hakuna maandamano yalioshuhudiwa nchini Mauritania kumpinga kiongozi huyo kama ilivyoshuhudiwa juma lililopita nchini Tunisia licha ya upinzani nchini humo kupinga ujio wake kwa sababu ya Saudi Arabia kuongoza mashambulizi nchini Yemen.

Nalo kundi la wasomi nchini humo, limekosoa ziara ya kiongozi huyo kwa kumhusiha na mauaji ya mwanahabari Jamal Kashoggi, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa kifalme nchini Saudi Arabia.

Awali Saudi Arabia ilisema mwandishi huyo aliuawa alipojaribu kupigana ndani ya ubalozi mdogo wa nchi hiyo Istanbul, nchini Uturuki.

Upande wa Rais Donald Trump baada ya kupata mashinikizo kutoka Congress kuwa kuna haja ya kuweka vikwazo dhidi ya Saudi hasa kukata mahusiano ya uuzaji silaha kwa Saudi,Trump alitoa kauli yake hivi karibuni kuwa anaishutumu Saudi Arabia kwa kutoa taarifa za uongo mwanzo wa tukio hili. Lakini akionesha kutoamini kama agizo la mauwaji lilitolewa na Prince Mohammed, akasema hakuna anayefahamu juu ya hili ,na hata mwili wa khashoggi hakuna anayejua ulipo.