rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

Congo Brazzaville Elimu

Imechapishwa • Imehaririwa

Mgomo wasitishwa katika Chuo Kikuu cha Brazzaville

media
Mji mkuu wa Congo, Brazzaville, ambako kunapatikana Chuo Kikuu cha Marien Ngouabi. Wikimedia/Jomako

Shughuli zimeanza tena katika Chuo Kikuu cha Marien Ngouabi mjini Brazzavile nchini Congo, baada ya miezi mitatu kufungwa kufuatia mgomo uliokuwa unaendelea.


Wafanyakazi ambao walikuwa wanadai malipo ya mishahara ya miezi sita wamekubaliwa kupewa malipo ya mwezi mmoja, kwa kusubiri mazungumzo zaidi na serikali.

Uamuzi wa kuendelea na shughuli katika Chuo Kikuu cha Marien Ngouabi ulichukuliwa mwishoni mwa mkutano mkuu uliofanyika siku ya Alhamisi alaasiri.

Maoni mbalimbali kuhusu kusitisha au la mgomo huo, hatimaye yalipelekea shughuli kuanza tena katika cho hicho leo Ijumaa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, vyama vya wafanyakazi vimetoa wito kwa wafanyakazi wote wa chuo kikuu kurejea kazini, baada ya makubaliano na serikali: Madai mbalimbali yamepatiwa suluhu ikiwa ni pamoja na "malipo ya mshahara ya mwezi wa Juni 2018; malipo ya masaa ya ziada ya mwaka wa mwaka 2016-2017, malipo ya ruzuku ya uendeshaji kazi, kuendelea na mazungumzo na Waziri mwenye dhamana ya Elimu ya Juu kwa lengo la kulipa mishahara ya miezi na masaa ya ziada ya mwaka 2017-2018 na kuundwa Kamati ya nadni itakayofuatilia utekelezaji wa ahadi walizoafikiana na serikali . "

Hatua ya kusitisha mgomo huo ilichukuliwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu na Waziri Mkuu Clement Mouamba.