rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Zimbabwe Robert Mugabe Emmerson Mnangagwa

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, hawezi kutembea

media
Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe alipoonekana mara ya mwisho mwezi Julai mwaka huu REUTERS/Siphiwe Sibeko

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, kwa sasa hawezi kutembea na yupo nchini Singapore kupata matibabu.


Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa amesema, Mugabe amefikia hatua hiyo kwa sababu ya umri wake mkubwa wa miaka 94, na afya yake inayoendelea kudhoofika.

“ Yeye (Mugabe) kwa sasa ni mzee. Hawezi kutembea lakini chochote anachokihitaji, tutampa,” aliwaambia Mamia ya wafuasi wa Mugabe katika eneo lake la Zvimba, Kilomita 100 kutoka jiji kuu la Harare.

Mugabe aliyeondolewa madarakani, mwaka mmoja uliopita, amekuwa hospitalini kwa miezi miwili sasa.

Mnangagwa amesema, serikali itaendelea kumhudumia Mugabe ambaye amwelezea kama baba wa taifa hilo la Kusini mwa bara la Afrika, aliyeongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30.