Pata taarifa kuu
DRC-UPINZANI-SIASA

Upinzani DRC wakutana Brussels kujaribu kuokoa umoja wao

Wanasiasa wa upinzani nchini DRC Jean-Pierre Bemba, Moise Katumbi, Adolphe Muzito na Martin Fayulu wanakutana Alhamisi hii Novemba 15 huko Brussels, siku tatu baada ya Felix Tshisekedi na Vital Kamerhe kujiondoa kwenye mkataba wa Geneva kuhusu uteuzi wa mgombea mmoja wa upinzani.

Jumatatu iliyopita, umoja wa upinzani ulivunjika baada ya Felix Tshisekedi (kyshoto) na Vital Kamerhe (kulia) kujiondoa kwenye mkaba wa Geneva, uliomteua Martin Fayulu kama mgombea pekee wa upinzani.
Jumatatu iliyopita, umoja wa upinzani ulivunjika baada ya Felix Tshisekedi (kyshoto) na Vital Kamerhe (kulia) kujiondoa kwenye mkaba wa Geneva, uliomteua Martin Fayulu kama mgombea pekee wa upinzani. Photo-Montage/RFI/© AFP
Matangazo ya kibiashara

Jean-Pierre Bemba, na Moise Katumbi Adolphe Muzito wanatarajia kuonyesha uungwaji wao mkono kwa mgombea wa upinzani Martin Fayulu, aliyeteuliwa Jumapili Novemba 11 kupeperusha bendera ya upinzani. Baada ya Vital Kamerhe na Felix Tshisekedi kujitoa kwenye mkataba wa Geneva, wanasiasa hao wtano wanatarajia kuokoa umoja wao ambao uko hatarini na kubitisha kwamba Martin Fayulu atabakia kuwa mgombea wao wa urais na kuwatolea wito wafuasi wao kumpigia kura mgombea wao.

Uteuzi wa mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 61 Martin Fayulu umekuja baada ya siku kadhaa za mazungumzo baina ya viongozi wakuu wa vyama saba vya upinzani yaliyofanyika mjini Geneva nchini Uswisi.

Martin Fayulu ataingia kwenye uchaguzi huo kutoshana nguvu na mgombea mteule wa serikali, bwana Emmanuel Ramazani Shadary ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani nchini humo.

Rais anayeondoka madarakani, Joseph Kabila, ameamua kutogombea tena muhula mwingine wa uongozi madarakani.

Martin mbali ya kujihusisha na masuala ya kisiasa ni mfanya biashara maarufu nchini Congo, miongoni mwa vitega uchumi vyake ni umiliki wa hoteli.

Martin Fayulu alisomea nchini Marekani, Ufaransa lakini pia aliwahi kufanya kazi katika makampuni makubwa ya simu nchini Marekani.

Alikuwa mstari wa mbele katika kumfanyia kampeni ya kisiasa aliyekuwa kiongozi wa upinzani marehemu Ettiene Tshisekedi.

Aliwahi kukamtwa mara kadhaa katika maandamano ya upinzani nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.