rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Karibu kesi 6,000 ya udhalilishaji wa kingono ziliripotiwa Uber nchini Marekani mwaka 2017 na 2018 (rasmi)

Eritrea UNSC

Imechapishwa • Imehaririwa

Umoja wa Mataifa waondoa vikwazo dhidi ya Eritrea

media
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeomba pia Eritrea na Djibouti kuendelea na juhudi zao. © REUTERS/Andrew Kelly

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeondoa vikwazo vyote dhidi ya Eritrea. Uamuzi ambao umepitishwa kwa kauli moja. Eritrea imekuwa ikikabiliwa na vikwazo vya silaha kwa kipindi cha miaka tisa.


Eritrea ilikuwa imewekewa vikwazo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vikwazo vya silaha, marufuku ya kusafiri, kuzuiliwa kwa mali za viongozi wa nchi hiyo katika nchi za kigeni.

Kwa upande wa Eritrea, wanasema vikwazo hivyo vilivyokuwa vikitumika kwa miaka tisa sasa vimepitwa na wakati na vimesalia tu kuwa ni historia kwa nchi hiyo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa likiishtumu Eritrea kwamba inaunga mkono wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabab nchini Somalia, madai ambayo Asmara imekuwa ikikanusha. Na hadi sasa, hakuna ushahidi wowote kuhusiana na madai hayo.

Kwa upande wa Umoja wa Mataifa wanasema kuondolewa kwa vikwazo hivyo ni njia ya kukaribisha uamuzi wa hivi karibuni wa Eritrea na Ethiopia wa kufufua uhusiano wao. Mwezi Julai, nchi hizo mbili zilitia saini makubaliano ya amani ya kihistoria ambayo yanakomesha miaka mingi ya migogoro kati ya nchi hizo.

Katika azimio lililopitishwa Jumatano wiki hii, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaomba Eritrea na Djibouti kuendelea na jitihada zao. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili hivi karibuni uliingiliwa na dosari, wakati mzozo wa mpaka kwenye eneo muhimu la Ras Doumeira umeendelea kuzigawanya nchi jizi mbili tangu mwaka 2008.

Pia Umoja wa Mataifa umeitaka Eritrea kutoa taarifa kuhusu hatima ya askari wa Djibouti ambao walitoweka baada ya mapigano miaka 10 iliyopita.