Pata taarifa kuu
DRC-UPINZANI-SIASA

Upinzani wagawanyika kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi DRC

Wafuasi wa chama cha UDPS nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekaribisha hatua ya kiongozi wao Felix Tshisekedi kujitoa kwenye mkataba wa viongozi wa upinzani wa uteuzi wa Martin Fayulu kama mgombea mmoja atakaye peperusha bendera ya upinzani.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha ECIDE,  Martin Fayulu.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha ECIDE, Martin Fayulu. AFP/Thierry Charlier
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili viongozi wakuu saba wa upinzani waliafikiana kumteua mgombea mmoja, Martin Fayulu, kuwania katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23. Mazungumzo kati ya wanasiasa hao yalifanyika mjini Geneva Uswisi. Hatua hiyo ilifuatia maandamano ya hasira yaliofanyika mapema Jumatatu mbele ya makao makuu ya vyama viwili vya upinzani.

Uteuzi wa Martin Fayul, kiongozi wa chama cha upinzani cha Ecidé umewashangaza wengi kwani hakuwa miongoni mwa watu mbao walikuwa wanapewa nafasi ya kuchukuwa na fasi hiyo hasa Felix Tshisekedi wa chama cha UDPS na Vital Kamerhe wa chama cha UNC.

Baadhi ya wafuasi wa chama cha UDPS "wamechoma moto picha za Felix Tshisekedi wakiacha zile za baba yake, Étienne Tshisekedi. Polisi wanajaribu kulinda usalama vilivyo, hapakuwa na tukio lolote baya shughuli zinaendelea kama kawaida, "msemaji wa polisi Kanali Pierrot Mwanamputu ameliambia shirika la Habari la AFP.

Wadadisi wanasema kwa sasa hatima ya upinzani nchini DRC iko matatani, ikiwa imesalia siku chache kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi. Uchaguzi wa urais na ule wa wabunge vimepangwa kufanyika Desemba 23. 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.