rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Karibu kesi 6,000 ya udhalilishaji wa kingono ziliripotiwa Uber nchini Marekani mwaka 2017 na 2018 (rasmi)

Eritrea UNSC

Imechapishwa • Imehaririwa

Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo dhidi ya Eritrea

media
Kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. REUTERS/Andrew Kelly

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kupiga kura Jumatano wiki hii kuondoa vikwazo vya silaha vilivyochukuliwa miaka kumi iliyopita dhidi ya Eritrea baada ya uamuzi wa nchi hiyo kufufua uhusiano na Ethiopia.


Wajumbe kutoka nchi kumi na tano wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walihitimisha mazungumzo yao siku ya Jumatatu na walikubaliana kuhusu rasimu ya azimio iliyotolewa na Uingereza ili kuondoa vikwazo vinvyoisibu Eritrea tangu mwaka 2009.

Wakati huo waangalizi wa Umoja wa Mataifa walibaini kwamba Eritrea inaunga mkono makundi yenye silaha nchini Somalia, madai ambayo mamlaka ya Eritrea ilifutilia mbali.

Ili kuidhinishwa, azimio hilo linapaswa kupata uungwaji mkono wa angalau kura tisa kati ya kumi na tano za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na bila hata hivyo kupingwa na kura yoyote ya veto ya wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo.

Azimio hilo pia linazitaka Eritrea na Djibouti kushirikiana kwa kuimarisha uhusiano wao na kutatua mgogoro wa mpaka unaozikabili nchi hizo kwa miaka kumi sasa.