Pata taarifa kuu
CAR-UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa yatoa msaada wa euro milioni 24 na silaha kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Ufaransaimekubali kutoa msaada wa euro milioni 24 na silaha kwa nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo inakabiliwa na machafuko na mdoroo wa usalama, amesema leo Ijumaa mjini Bangui Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian akaribishwa na mwenzake wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Charles Armel Doubane huko Bangui Novemba 1, 2018.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian akaribishwa na mwenzake wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Charles Armel Doubane huko Bangui Novemba 1, 2018. Gael GRILHOT / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ufaransa inataka kuendelea na ushirikiano wake wa kihistoria na Jamhuri ya Afrika ya Kati," Le Drian amesema katika mkutano na waandishi wa habari mjini Bangui ambapo aliwasili siku ya Alhamisi.

Bw Le Drian ametia saini kwenye mkataba kuhusu msaada wa euro milioni 24 mnamo mwaka 2018 ikiwa ni pamoja na kuchangia kwa malipo ya mishahara na malimbikizo ya pensheni, kuendeleza maeneo jirani na Cameroon yanayokumbwa na wimbi la wakimbizi kujenga madaraja ya ili kurahisishia katika kanda hiyo.

Waziri wa mambo ya Nje aw Ufaransa pia ametangaza kuwa hivi karibuni Paris itaipa silaha Jamhuri ya Afrika ya Kati, ikiwa ni pamoja na bunduki 1400 kwa kufadhili jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA).

Ili kurejesha amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Le Drian ameelezea msimamo wa Ufaransa kwamba "hakuna njia mbadala kwa mpango wa amani wa Umoja wa Afrika". "Tunapaswa kutekeleza sasa," amesema. "Wale ambao wana mawazo mengine, wale ambao wana ajenda nyingine watalazimika kutii amri," ameonya.

Upatanishi wa Umoja wa Afrika (AU) uliyozinduliwa mnamo mwezi Julai 2017 na kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa na washirika wakuu wa Jamhuri ya Afrika ya Katini unakosolewa na wanadiplomasia na waangalizi kwa jinsi unavyondeshwa kwa mwendo wa kinyonga na kutokuwa na nguvu.

Tangu mwaka 2013, karibu eneo lote la Afrika ya Kati limekuwa chini ya udhibiti wa makundi ya watu wenye silaha, katika nchi yenye wakazi milioni 4.5 na mabyo imewekwa miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani lakini tajiri kwa almasi, dhahabu na uranium.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.