rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Somalia ISIL Afrika

Imechapishwa • Imehaririwa

Mmoja wa viongozi wa Islamic State auawa nchini Somalia

media
Bendera ya Islamic State Reuters

Ripoti kutoka Somalia zinaeleza kuwa kiongozi wa pili wa kundi la kigaidi la Islamic State nchini humo, ameuawa mjini Mogadishu.


Shirika la Habari la Uingereza la BBC, linaeleza kuwa Mahad Moallim alikuwa katika orodha ya magaidi sugu wanaotafutwa na Marekani.

Duru zinasema kuwa, Moallim amepigwa risasi na watu waliokuwa na silaha wanaominiwa kuwa wafuasi wa Islamic State.

Aidha, inaelezwa kuwa mauaji haya yametokana na mzozo wa uongozi ndani ya kundi hilo nchini Somalia baada ya kiongozi wake kuwa na hali mbaya ya kiafya.

Magaidi hao wanaofahamika nchini humo kama Daish, wanatazamwa kama wapinzani wa Al Shabab na wanakadiriwa kuwa kati ya 400-500 na ngome yao ni jimbo la Puntland.