Pata taarifa kuu
CAR-HAKI-USALAMA

Mahakama Maalumu yazinduliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, imezindua rasmi mahakama maalumu itakayoshughulikia makosa ya uhalifu yaliyotekelezwa nchini humo kwa nyakati tofauti.

Jaji wa Mahakama Maalum ya Uhalifu (CPS) Michel Landry Louanga, aliyeteuliwa kuwa rais wa taasisi hiyo, afungua kikao cha kuanzisha rasmi kazi ya Mahakama nchini CAR, Oktoba 22, 2018.
Jaji wa Mahakama Maalum ya Uhalifu (CPS) Michel Landry Louanga, aliyeteuliwa kuwa rais wa taasisi hiyo, afungua kikao cha kuanzisha rasmi kazi ya Mahakama nchini CAR, Oktoba 22, 2018. Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kikao cha kwanza cha mahakama hii kilifanyika siku ya Jumatatu chini ya majaji 13 wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na 12 kutoka jumuiya ya kimataifa, ambapo watakuwa na jukumu la kusikiliza kesi ya makosa yaliyotekelezwa kuanzia mwaka 2003.

Katika miezi ya hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati Faustin-Archange Touadera aliyashutumu makundi ya wapiganaji yanayopambana na walinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.

Rais Faustin-Archange Touadera alisema makundi hayo yamekuwa wakifanya uhalifu, hali iliyosababisha watu wengi kukamatwa mateka.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, yamesababisha mamia ya raia kuuawa na wengine maelfu kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.