rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Cameroon Paul Biya

Imechapishwa • Imehaririwa

Matokeo ya uchaguzi wa urais kutangazwa Jumatatu hii Cameroon

media
Wananchi wa Cameroon wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa urais. ALEXIS HUGUET / AFP

Baraza la Katiba linatarajia kutatangaza Jumatatu hii, Oktoba 22 matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 7 nchini Cameroon. Hata hivyo upinzani ulijaribu kuandamana katika mji wa Douala siku ya Jumapili, lakini vikosi vya usalama viliweza kuzima maandamano hayo.


Upinzani unasema unasubiri kupinga udanganyifu wa kura uliogubika uchaguzi huo, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na upinzani ambacho hakikutaja jina.

Wadadisi wanasema Paul Biya anatarajia kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo.

Maandamano ambayo yalikuwa yamezuiliwa na serikali Jimbo la Doualayalizimwa na vikosi vya usalama. Mapema asubuhi, nyumba ya mbunge Jean Michel Nitcheu kutoka chama cha SDF, ambaye alikuwa mmmoja kati ya waandaaji wakuu wa maandamano hayo, ilizingirwa na maafisa kadhaa wa polisi. Mmoja wa ndugu zake amethibitisha kwamba hakuweza kuondoka nyumbani kwake.

Idadi kubwa ya polisi pia ilishuhudiwa nyumbani kwa Édith Kah Wallah wa Chama cha Cameroon People's Party. Katika video ambayo ilirushwa kwenye mitandao ya kijamii, alionekana akibishan ana maafisa wa polisi ambao walikuwa mbele ya nyumba yake. Eneo ambapo waandamanaji walitarajiwa kukusanyika pia lilizingirwa na polisi.

Hali ya utulivu ilishuhudiwa katika mji wa Yaounde.

Matokeo ya uchaguzi wa urais yamepangwa kutangwa saa 11 mchana saa za Cameroon.