Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Waasi wa ADF waua raia 11 na kuteka 15 kwenye mji wa Beni

Waasi wenye silaha wamewaua watu 11 na kuwateka wengine 15 wakiwemo watoto 10, katika shambulio walilotekeleza usiku wa kuamkia leo kwenye mji wa Beni mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo.

Picha ya maktaba ikiwaonesha wanajeshi wa Serikali ya DRC wanaopambana na wapiganaji waasi mashariki mwa nchi hiyo
Picha ya maktaba ikiwaonesha wanajeshi wa Serikali ya DRC wanaopambana na wapiganaji waasi mashariki mwa nchi hiyo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Polisi kwenye mji huo wanasema wamefanikiwa kupata miili 11 ya raia waliouawa kwenye mji wa Matete kaskazini mwa Beni na kuongeza kuwa watoto waliotekwa wana kati ya umri wa miaka 5 hadi 10.

Msemaji wa jeshi la Serikali la FARDC, Mak Hazukay, amesema wanahofia kuwa wapiganaji waasi wa Uganda wa ADF ndio wamehusika katika shambulio hilo.

Kwenye taarifa yake jeshi limesema baada ya kupokea taarifa kuhusu mashambulizi haya, kikosi maalumu kilitumwa na kufanikiwa kuwadhibiti wapiganaji, ambapo imeongeza kuwa miongoni mwa waliouawa wamo pia wanajeshi wa Serikali.

Wakazi wa mji wa Matete walioshuhudia mashambulizi hayo, wamethibitisba kushuhudia miili ya wanajeshi wawili wa Serikali kwenye eneo la tukio.

Awali kabla ya taarifa ya jeshi la Serikali, msemaji wa jeshi la walinda amani wa umoja wa mataifam, alithibitisha vikosi vyao kukabiliana na wapiganani waliokuwa na silaha jirani na mji wa Beni kwenye eneo linalopakana na nchi ya Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.