rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Gambia Adama Barrow Yahya Jammeh

Imechapishwa • Imehaririwa

Gambia yazindua Tume ya Ukweli Haki na Maridhiano

media
Rais wa Gambia Adama Barrow REUTERS/Benoit Tessier

Gambia imezindua Tume ya Ukweli Haki na Maridhiano, kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyotokea wakati wa rais wa zamani Yahya Jammeh.


Tume hiyo hiyo itakuwa na Makamishena 11 ambao tayari wameapishwa jijini Banjul kuanza kazi hiyo.

Kuanzia mwisho wa mwezi Oktoba, watu mbalimbali walioteswa au kunyanyaswa wanatarajiwa kwenda kutoa ushahidi wao mbele ya Tume hiyo.

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema raia wa nchi hiyo walioteswa, kubakwa wakiwa jela au kulazimishwa kunywa dawa zilizotengezwa na Jammeh ili kuponya maambukizi ya Ukimwi watajitokeza kutoa shuhuda zao.

Rais Adama Barrow amesema kuwa, Tume hiyo itasaidia sana katika uponyaji wa nchi hiyo.

“ Tusimame pamoja kusema, hatutaruhusu tena watu wachache kututesa kama taifa,' aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Tume hii kama ilivyokuwa ile ya Afrika Kusini, itasikiliza shuhuda dhidi ya watu mbalimbali kipindi chote cha miaka 22 alichoongoza Jammeh ambaye amepewa hifadhi nchini Equitorial Guinea.