rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Gambia Yahya Jammeh Adama Barrow

Imechapishwa • Imehaririwa

Tume ya kuchunguza yaliyotendwa na utawala wa Jammeh kuzinduliwa

media
Aliye kuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins/Files

Zaidi ya miezi 20 baada ya rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh kulazimishwa kwenda uhamishoni, nchi hiyo inazindua rasmi Jumatatu wiki hii tume itayotoa mwanga kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa chini ya utawala wa kiongozi huyo.


Lakini uwezekano wa kumhukumu Yahya Jammeh, askari wa zamani, ambaye alitawala Gambia, nchi ndogo ya Afrika Magharibi, kwa muda wa miaka 22, bado hatua hiyo inaleta utata.

Wajumbe 11 wa Tume ya "Ukweli, Maridhiano na Kuwafidia Wahanga" (TRRC kwa Kiingereza) iliyozinduliwa mwaka 2017 na mrithi wake Adama Barrow, hatimaye wanatarajia kula kiapo Jumatatu wiki hii, Waziri wa Sheria, Abubacarr Tambadou ametangaza.

Vikao vya hadhara vya Tume ya Ukweli, Maridhiano na Kuwafidia Wahanga, vitaanza muda mfupi baada ya sherehe hiyo, Bw Tambadou amesema.

Tume hiyo ambayo inaoongozwa na mwanadiplomasia wa zamani kwenye Umoja wa Mataifa, Lamin Sise, inajumuisha wanawake wanne, ikiwa ni pamoja na makamu wa rais Adelaide Sosseh, na inaundwa na watu kutoka jamii zote za kikabila na za kidini nchini.

Watetezi wa haki za binadamu wanashtumu utawala wa Yahaya Jammeh kwamba ulihusika katika mateso dhidi ya wanasiasa wa upinzani na waandishi wa habari, mauaji ya watu waliokuwa mikononi mwa maafisa wa serikali, kukamatwa na kufungwa bila hatia na visa vya watu kutoweka.