Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Upinzani waitisha maandamano dhidi ya mchakato wa uchaguzi DRC

Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC (CENI) na wagombea wa upinzani bado hawajakubaliana kuhusu mfumo wa uchaguzi utakaotumiwa katika uchaguzi wa Desemba 23.

Martin Fayulu, mgombea wa urais (picha ya kumbukumbu, 2016).
Martin Fayulu, mgombea wa urais (picha ya kumbukumbu, 2016). AFP/Thierry Charlier
Matangazo ya kibiashara

Hata tume ya kiufundi inayotakiwa kuwezesha mazungumzo kati ya wagombea na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) bado haijawekwa.

Wakati huo huo viongozi wa upinzani siku ya Alhamisi wiki hii waliwataka wafuasi wao kuandamana tarehe 26 Oktoba mwaka huu kupinga katu katu matumizi ya mashine za kupigia kura na kuomba uchapishaji wa kadi za kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 23 Desemba.

Wagombea wa upinzani hawako tayari kukabiliana na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), kuunda tume ya ufundi ambayo inatakiwa kuwezesha mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali nyeti kabla ya uchaguzi wa urais wa Desemba 23.

Katika mkutano wao siku ya Alhamisi mjini Kinshasa, wagombea hao walihoji mambo mawili ya lazima. Martin Fayulu, mgombea urais, alisoma taarifa iliyotiliwa saini na wawakilishi wa viongozi wakuu wa upinzani: "upinzani unatoa madai yake yanayoendana na maswali mawili muhimu, ikiwa ni pamoja na uhalali wa mashine za kupigia kura na kufuta wapiga kura milioni 10 ambao imegundulika kuwa kwenye daftari la kupigia kura hakuna alama zao za vidole, kabla ya kuundwa kwa tume ya kiufundi. "

Licha ya mgogoro huu wa kutokuwa na imani na Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), upinzani haujatishia kususia uchaguzi, na mpaka sasa unaona kuwa njia rahisi na halali ni kuchapisha kadi za kupigia kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.