rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Liberia Charles Taylor

Imechapishwa • Imehaririwa

Mke wa zamani wa Charles Taylor akana mashitaka yanayomkabili

media
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor. REUTERS/Vincent Jannink/Pool

Agnes Reeves Taylor, aliyekuwa mke wa Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor, amekana mashtaka ya mateso wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Liberia katika miaka ya 1990, wakati alipokuwa akisikilizwa mbele ya mahakama ya jinai ya London, nchini Uingereza.


Agnes Reeves Taylor, mwenye umri wa miaka 52, anatuhumiwa kuhusika katika vitendo vya mateso dhidi ya watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na watoto, " alipokuwa akishikiliwa nyadhifa mbalimbali."

Pia anatuhumiwa kuwa alishinikiza majeshi ya Charles Taylor, National Patriotic Front of Liberia (NPFL), kutumia ubakaji wa wanawake kama njia ya mateso.

Agnes Reeves Taylor, aliyekuwa mhadhiri katika Chuko Kikuu cha English Coventry University, anaishi katika mji wa Dagenham, mashariki mwa London, na kwa sasa yuko chini ya ulinzi katika gereza la Bronzefield, kusini-mashariki mwa Uingereza.

Kesi yake inaweza kufunguliwa mnamo mwezi Januari mwakani.

Charles Taylor na Agnes Reeves Taylor walitalakiana mnamno mwaka 1996. Kisha kiongozi huyo wa waasi alichukua hatamu ya uongozi kama rais wa Liberia kuanzia mwaka 1997 hadi 2003. Alihukumiwa na Mahakama Maalum ya Sierra Leone (SCSL) katika miaka ya 2012 kifungo cha miaka 50 kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa katika nchi jirani ya Liberia ya Sierra Leone.

Charles Taylor anatumikia kifungo cha miaka hamsini katika jela la Uingereza.

Charles Taylor alihukumiwa na Mahakama Maalum ya Sierra Leone (SCSL) katika miaka ya 2012 kifungo cha miaka 50 kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa katika nchi jirani ya Liberia ya Sierra Leone. (Photo : AFP/ Carte : RFI / Montage : G. Ngosso )