rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Libya ISIL

Imechapishwa • Imehaririwa

Miili ya watu 77 yapatikana katika kaburi la pamoja Sirte, Libya

media
Mpiganaji anayeunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa katika mji wa Sirte, Libya, Agosti 14, 2016. AFP

Miili 75 ya binadamu iliyoanza kuoza imepatikana katika kaburi la pamoja katika eneo linaloaminiwa kuwa ngome ya kundi la kigaidi la Islamic State, Magharibi mwa mji wa Sirte.


Maafisa wa serikali wanashuku kuwa, miili hiyo ni ya wafuasi wa Islamic State.

Mji huo wa Pwani umekuwa, ngome ya Islamic State baada ya kuanza kwa vita mwaka 2011 vilivyomwondoa madarakani aliyekuwa kiongozi Muamar Kadhafi.

Hivi karibuni mapigano makali karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli yalishuhudiwa kati ya makundi hasimu na kusababisha watu wengi kuyahama makaazi yao, huku idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka kila kukicha.

Libya imeendelea kukumbwa na mdororo wa usalama, huku serikali dhaifu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ikishindwa kurejesha usalama katika baadhi ya maeneo ya nchi.