Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Askari nane wa Chad wauawa katika mapigano na Boko Haram

Askari nane wa Chad wameuawa katika Jimbo la Ziwa Tchad katika mapigano na wapiganaji wa kundi la Boko Haram, ambalo limepoteza wapiganaji wake 48 katika mapigano hayo, kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi.

Helikopta za jeshi la Chad zikipiga kambi karibu na mji wa Gamboru.
Helikopta za jeshi la Chad zikipiga kambi karibu na mji wa Gamboru. AFP PHOTO / STEPHANE YAS
Matangazo ya kibiashara

"Magaidi wa Boko Haram walishambulia mapema leo asubuhi ngome ya vikosi vya ulinzi katika mji wa Kaiga Kindji", msemaji wa kijeshi katika mji wa N'Djamena Kanali Azem ameliambia shirika la Habari la AFP.

Msemaji huyo wa jeshi ameongeza kuwa shambulio hilo lilirejeshwa nyuma na askari 8 wameuawa na wengine 11 wamejeruhiwa, na "magaidi 48 wameuawa katika mapigano hayo.

Ingawa Chad haikabiliwa sana na mashambulizi ya Boko Haram ikilinganishwa na nchi jirani ya Nigeria, machafuko yanayosababishwa na Boko Haram yaliongezeka nchini humo hivi karibun, baada ya hali ya utulivu kurejea.

Mapema mwezi Oktoba, Boko Haram ilizindua mashambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi katika mji wa Litri, kilomita 4 na mpaka wa Nigeria katika Jimbo la Ziwa Chad. Wakati huo askari mmoja wa Chad aliuawa.

Mwishoni mwa Septemba, watu sita, ikiwa ni pamoja askari wawili waliuawa katika shambulio katika mwambao wa Ziwa Chad Ziwa, shambulio lililoendeshwa na Boko Haram, ambayo ilipoteza wanajihadi 17 waloiuawa na jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.