Pata taarifa kuu
CAMEROON-UCHAGUZI-USALAMA

Maurice Kamto adai ameshinda uchaguzi wa urais Cameroon

Siku moja baada ya uchaguzi wa urais nchini Cameroon, wakati matokeo ya awali ya uchaguzi yakiendelea kusubiriwa, Maurice Kamto, mmoja wa wagombea wakuu ametangaza kwamba ameshinda uchaguzi.

Maurice Kamto katika mkutano na waandishi wa habari ambapo amedai kuwa ameshinda uchaguzi wa urais, Oktoba 8, 2018 Yaounde.
Maurice Kamto katika mkutano na waandishi wa habari ambapo amedai kuwa ameshinda uchaguzi wa urais, Oktoba 8, 2018 Yaounde. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Maurice Kamto amesema kuwa ameshinda uchaguzi wa urais katika duru ya kwanza. Waziri wa zamani wa Paul Biya ametoa mfano wa mchezo wa soka na kusema ameshinda. Hata hivyo, hakutoa takwimu wala asilimia ya kura alizopata.

"Nilipata nafasi ya kupachika bao na kupata ushindi wa kihistoria kupitia mkwaju wa penalti. Nilipiga mkwaju na nikafunga bao, "Maurice Kamto amesema mbele ya wafuasi wake na waandishi wa habari waliokusanyika kwa mkutano wa waandishi wa habari.

Maurice Kamto ametangaza kwamba ameshinda uchaguzi huku wafuasi wake wakipiga makofi na kufurahia ushindi huo.

Rais Paul Biya hajazungumza chochote kuhusiana na madai hayo, lakini chama chake kimepuuzia mbali madai ya Maurice Kamto. Kwa upande wa Jacques Fame Ndongo, Waziri wa Elimu ya Juu na Katibu wa Mawasiliano wa chama cha RDPC, chama tawala, amesema madai hayo ni uzushi, na hayana nguvu yoyote.

Akihojiwa na RFI, mgombea wa chama cha SDF, Joshua Osih amesema anastaajabishwa na madai yaMaurice Kamto kwa sababu kwa mujibu wa Bw Osih inachukua muda kwa kukusanya matokeo yote. "Sisi ni chama cha kisiasa cha upinzani ambacho kilikuwa na wawakilishi wengi katika vituo vya kupigia kura. Kwa sasa, ni vigumu kupata asilimia ishirini kutoka vituo vya kupigia 25,000.

Wapiga kura milioni 6.6 walipiga kura Jumapili Oktoba 7 nchini Cameroon kumchagua rais wao mpya. Wagombea nane walishiriki kinyang'anyiro hicho, ikiwa ni pamoja na rais anaye maliza muda wake Paul Biya. Uchaguzi ambao ulifanyika katika hali ya utulivu, isipokuwa katika maeneo mawili yanayozungumza Kiingereza.

Matokeo yanatarajiwa kufahamika, baada ya wiki mbili, katika Uchaguzi ambao rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 85, akitarajiwa kushinda na kuendeleza uongozi wake wa miaka 36.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.