rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Cameroon Paul Biya

Imechapishwa • Imehaririwa

Uchaguzi wa urais Cameroon: Hali ya taharuki yaendelea katika maeneo yanayozungumza Kiingereza

media
Askari akitoa ulinzi kabla ya zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa urais huko Mwangai karibu na Buea katika eneo la linalozungumza Kiingereza. MARCO LONGARI / AFP

Wapiga kura milioni 6.6 walipiga kura Jumapili Oktoba 7 nchini Cameroon kumchagua rais wao mpya. Wagombea nane walishiriki kinyang'anyiro hicho, ikiwa ni pamoja na rais anaye maliza muda wake Paul Biya. Uchaguzi ambao ulifanyika katika hali ya utulivu, isipokuwa katika maeneo mawili yanayozungumza Kiingereza.


Kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters matukio kadhaa ya ghasia yalishuhudiwa wakati wa zoezi la upigaji kura lilipoanza katika uchaguzi uliotarajiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza muda wa utawala wa Rais Paul Biya, mmoja wa viongozi wa Afrika aliye madarakani kwa muda mrefu.

Shirika la habari la Reuters lilieleza kwamba zoezi la upigaji kura lilifanyika salama kwa sehemu kubwa ya nchi hiyo ya Afrika ya kati inayokumbwa na mgawanyiko wa lugha na kupelekea baadhi ya vituo vya kupiga kura kutofunguliwa katika maeneo yanayozungumza Kiingereza na kuzusha ghasia.

Watu watatu waliokuwa na silaha kwenye eneo linalojitenga walifyatuliwa risasi na kuuwawa na vikosi vya usalama huko kaskazini mashariki katika mji wa Bamenda unaozungumza lugha ya Kiingereza, kwa mujibu wa chanzo cha usalama.

Hata hivyo Rais anaye maliza muda wake Paul Biya amekaribisha hali ya utulivu iliyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi katika sehemu kubwa ya nchi.

Vituo vingi vya kupigia kura havikufungua kutokana na mdororo wa usalama, na baadhi vilihamishwa hadi kilomita 45, lakini licha kufunguliwa hakuna mpiga kura hata mmoja ambaye alijitokeza kuja kupiga kura.

Kwa jumla ya vituo vya kupigia kura 306, 13 peke ndivyo vilifunguliwa Jumapili huko Bamenda.

Matokeo yanatarajiwa kufahamika, baada ya wiki mbili, katika Uchaguzi ambao rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 85, akitarajiwa kushinda na kuendeleza uongozi wake wa miaka 36.