Pata taarifa kuu
LIBYA-MISRI-USALAMA

Kiongozi wa wanamgambo wa Kiislam akamatwa Libya

Vikosi vya Mashariki mwa Libya vinamshikilia tangu Jumatatu asubuhi Hicham Al-Achmawi, afisa wa zamani wa jeshi la Misri ambaye ni kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu wenye silaha.

Hicham Al-Achmawi kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu wenye silaha aliyetangaza kumg'oa madarakani rais aw Misri Al Sisi kuptia vita vitakatifu.
Hicham Al-Achmawi kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu wenye silaha aliyetangaza kumg'oa madarakani rais aw Misri Al Sisi kuptia vita vitakatifu. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii, ambayo ilitolewa na msemaji wa jeshi la Libya, imethibitishwa na janzo cha kijeshi cha Misri, kwa mujibu wa shirika la Habari la Reuters.

Mtu huyo, raia wa Misri, ambaye alikuwa akisakwa na vyombo vya usalama na ulinzi amekamatwa huko Derna, ambapo majeshi ya mashariki mwa lIbya yanapigana na makundi ya kijihadi, amesema Ahmed Mismari, msemaji wa kundi moja la wapiganaji (ANL), linalodhibiti eneo la Cyrenaica.

Kuna uwezekano Achmaoui kukabidhiwa mamlaka ya Misri wakati idara ya usalama ya Libya itakuwa imekamilisha uchunguzi wake.

Kundi la wapiganaji la ANL limechapisha picha ya Achmaoui akiwa amejaa damu kwenye uso.

Kiongozi huyo wa wanamgambo wa Kiislamu, ambaye alijiita Abu Omar al Muhajir al Masri anaongoza mtandao wa Ansar al-Islam, kundi ambalo lilidai kuhusika na shambulizi baya dhidi ya polisi wa Misri katika jangwa nchini humo mnamo Oktoba 2017.

Serikali ya Misri inashtumu kundi hilo,kuwa lina mafungamano na kundi la Al Qaeda, kwa kujaribu kumua waziri wa zamani wa mambo ya ndani mnamo mwaka 2013.

Katika miaka ya hivi karibuni, mtandao huu wa Achmaoui umefanya kampeni ya kuajiri miongoni mwa maafisa wa jeshi na polisi wa Msri. Kwa upande wa idara ya upelelezi na usalama nchini misri, Achmaoui ni hatari zaidi kuliko Waislam wanaopigana katika rasi ya Sinai ya Misri.

Mnamo mwezi Julai 2015, kwa mujibu wa mtandao wa makundi ya wanamgamo wa Kiislamu, SITE, katika ujumbe wa maneneno, Achmaoui altoa wito wa kupindua kupitia vita vtakatifu "Firauni" Abdel Fattah al-Sisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.