Pata taarifa kuu
NIGERIA-SIASA-USALAMA

Atiku Abubakar kupambana na Buhari katika uchaguzi wa urais Nigeria

Chama kikuu cha upinzani nchini Nigeria PDP, kimemchagua aliyekuwa Makamu wa rais Atiku Abubakar kuwa mgombea wake kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Februari mwaka ujao.

Makamo wazamani wa rais Atiku Abubakar atuliwa kupeperisha bendera ya chama kikuu cha upinzani cha PDP katika uchaguzi wa urais.
Makamo wazamani wa rais Atiku Abubakar atuliwa kupeperisha bendera ya chama kikuu cha upinzani cha PDP katika uchaguzi wa urais. AFP/PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Abubakar mwenye umri wa miaka 71, sasa atakuwa mpinzani Mkuu wa rais Muhamadu Buhari anayewania nafasi kwa muhula wa pili.

Rais Buhari naye amekubali uteuzi wa chama chake cha APC, na kuwaambia raia wa nchi hiyo kuwa hatawaangusha iwapo watamchagua tena.

Mbali na Atiku na rais Buhari, wagombea wengine 9 watawania wadhifa huo.

Hivi karibuni Rais Muhammadu Buhari alitangaza kuwa atagombea tena kiti cha urais katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika Februari mwaka ujao wa 2019.

Buhari ambaye aliingia madarakani mwaka 2015 kwa ahadi za kutokomeza ufisadi nchini Nigeria ambayo ni kubwa kiuchumi na wingi wa idadi ya watu barani Afrika amekuwa akikosolewa mno na wapinzani wake kutokana na kile wanachosema kuwa, ameshindwa kutekeleza ahadi zake.

Aidha wapinzani wa Rais Buhari wanasema kuwa, kiongozi huyo ameshindwa kuliangamiza kundi la kigaidi la Boko Haram kwani moja ya ahadi zake kuu katika kampeni za uchaguzi ilikuwa ni kukabiliana na magaidi hao ambao wamesababisha maafa makubwa katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika na hata katika nchi jirani kama Cameroon, Niger na Chad.

Kwa sasa uchumi wa Nigeria unalegalega, ukosefu wa ajira na umasikini vimeongezeka huku kukiwemo na tatizo kubwa la ufisadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.