Ajali yaua watu 60 magharibi mwa DRC
Zaidi ya watu hamsini wamefariki dunia baada ya lori la mafuta kugongana na gari kwenye barabara kuu magharibi mwa DRCongo huku zaidi ya mia wakijeruhiwa kufuatia moto mkali uliozuka.
Imechapishwa:
Ajali hiyo ilitokea katika barabara inayounganisha mji wa kinshasa na bandari ya matadi.
Atou Matabuana,kiongozi wa jimbo la kati amesema takribani watu mia moja wamepata majeraha baada ya kuungua moto.
Aidha imefahamika weengine saba wakifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali ya sent luc huko kisantu mji wa jirani.
Kwa mujibu wa UN Radio Okapi moto uliwaka kwa kasi na kusambaa ghafla katika nyumba jirani.
Barabara nyingi katika mataifa ya Afrika ya kati zimesahaulika baada ya kushuhudia miaka mingi ya vita jambo linalotajwa kuchangia ajali nyingi kutokea.